toleo jipya : Tor Browser 10.5

Tor Browser 10.5 sasa inapatikana kutoka Tor Browser pakua ukurasa na saraka zinazosambaza. toleo la android pia inapatikana kwenye Google Play na inapaswa kupatikana kwenye F-Droid ndani ya siku inayofuata.

Nakala hii inajumuisha toleo muhimu la usalama kwa Firefox.

Utoaji mpya wa Tor Browser unalenga kuboresha upatikanaji wa mtandao kwa watumiaji wanaounganisha kupitia Tor katika mazingira yaliyodhibitiwa.

kipi kipya?

#### V2 Oion Service imepungua thamani

Kama tulivyotangaza mwaka jana,huduma ya Tor services vya aina ya v2 zitakuwa hazipatikani tena mara tu Tor Browser itakapoanza kutumia Tor 0.4.6.x mwezi Oktoba 2021. Kuanzia sasa hadi wakati huo, Tor Browser kitakuonya unapotembelea tovuti ya onion ya aina ya v2 juu ya upungufu wake unaokuja.

Snowflake sasa inapatikana kama kiungio

Kwa kutumia Snowflake, watumiaji wanaodhibitiwa wanaweza kutegemea proxies unaoendeshwa na watu wanaojitoleankwa ajili ya kuunganisha na mtandao.

Katika robo ya kwanza ya mwaka huu, timu ya UX iliendesha utafiti kwenye Tor Browser Alpha ili kuelewa vizuri uzoefu wa watumiaji wa Snowflake. Utafiti huo ulipokea majibu kamili 1,795, ambapo washiriki 726 walithibitisha kutumia Snowflake kama njia pluggable transport. Watumiaji wengi wa Snowflake ambao walikamilisha uchunguzi walianza kutumia Tor Browser mara kadhaa kwa wiki ndani ya mwaka uliopita. 75% ya watumiaji walikuwa na maoni chanya juu ya Snowflake, ingawa wengi wao walipata matatizo ya uunganisho na kasi ndogo wakati wa kuvinjari. Ukweli huu na mtandao thabiti wa wanaojitolea unaturuhusu kuifanya ipatikane kwenye toleo hili.

Kuboresha uzoefu wa mtumiaji wa kuunganisha kwenye Tor

Tor Launcherimekuwa jukwaa la chaguo za hali ya juu za mtandao wa Tor kwa miaka kadhaa. Nayo pia hutumika kama sehemu ya udhibiti kwa watumiaji ambao wako kwenye mitandao iliyodhibitiwa. Timu za UX na isiofanya udhibiti wa mtandao ziliunganisha juhudi zao ili kuboresha mtiririko wa kuunganisha kwa watumiaji Tor Browser. Nakala hii ni ya kwanza katika safu inayokuja ya kuwasaidia watumiaji waliofungiwa kupata mtandao wazi kwa urahisi kwa mtiririko wa uunganisho, kugundua udhibiti na kutoa viungio.

vitu vinavyojulikana

Tor browser 10.5 inakuja na masuala kadhaa yanayojulikana:

toa mrejesho

Ikiwa una mapendekezo juu ya jinsi tunavyoweza kuboresha toleo hili, tafadhali tujulishe. Asante kwa timu zote katika Tor, na kwa wale wengi waliojitolea, ambao wamechangia kwa toleo hili.

Unaitaji msaada?

Angalia FAQ katika jamii yetu

Tembelea Msaada

Wasiliana

wasiliana na sisi moja kwa moja!

Jiunge nasi kwenye IRC