Hii toleo jipya linategemea vipengele vilivyowekwa Tor Browser 10.5 ili kubadilisha uzoefu wa mtumiaji wa kuunganisha kwenye Tor kutoka maeneo yaliyodhibitiwa kwa nguvu.

kipi kipya?

Tor Browser 11.5

utambuzi na ukwepaji wa udhibiti wa moja kwa moja

Tulianza kubadilisha uzoefu wa kuunganisha kwenye Tor tangu kuzinduliwa kwa Tor Browser 10.5mwaka jana, ikiwa ni pamoja na kuisha muda kwa Tor Launcher na kuiunganisha mchakato wa kuunganisha kwenye kivinjari cha kompyuta. Hata hivyo, kukwepa udhibiti wa Mtandao wa Tor yenyewe bado ilibaki kuwa mchakato wa hatua inayochanganya - kuhitaji watumiaji kuingia kwenye mipangilio ya Mtandao wa Tor na kujua wenyewe jinsi ya kutumia daraja ili kuondoa kizuizi cha Tor. Zaidi ya hayo, ukaguzi wa Tor hauna uwiano - na wakati mtindo fulani wa pluggable Transport au usanidi wa bridge unaweza kufanya kazi katika nchi moja, hiyo haimaanishi itafanya kazi mahali pengine.

Neno hili liliwawekea vikwazo watumiaji waliodhibitia (ambao tayari wapo chini ya shinikizo kubwa) kufikiria ni chaguo gani la kuchagua, hivyo kusababisha majaribio mengi, makosa na mafadhaiko katika mchakato huo. Kwa kushirikiana na kikosi cha kuzuia udhibiti katika Tor project, tumekuwa tukijitahidi kupunguza mzigo huu kwa kuanzishaConnection Assit : kipengele kipya ambacho kinaahidi kutoa usaidizi wa kuwezesha mazingira ya bridge kusanidi kazi vizuri zaidi katika eneo lako.

Connection Assist

Connection Assist inafanya kazi kwa kutafuta na kupakua orodha ya chaguo za nchi maalum zenye sasisho la hivi karibuni ili kujaribu kutumia mahali ulipo (kwa idhini yako). Inasimamia kufanya hivyo bila kuhitaji kuunganisha kwanza kwenye Mtandao wa Tor kwa kutumia moat - chombo kile cha kutanguliza kikoa kinachotumiwa na Kivinjari cha Tor kuomba bridge kutoka torproject.org.

Wakati Connection Assist imefikia hatua ya kihistoria ya kutolewa rasmi kwa mara ya kwanza, hii ni toleo la 1.0 pekee, na maoni yako yatakuwa muhimu sana katika kusaidia kuiboresha uzoefu wa mtumiaji katika matoleo ya baadaye. Watumiaji kutoka nchi ambazo Mtandao wa Tor unaweza kuzuiwa (kama vile Belarus, China, Russia na Turkmenistan) wanaweza kujaribu toleo jipya zaidi la kipengele hiki kwa kujitolea kama jaribio la alpha, na kutoa taarifa ya matokeo yako kwenye jukwaa la Tor ili kusaidia katika upimaji.

kutengeneza upya mpangilio wa mtandao wa Tor

unganisha mpangilio](/static/images/tb115/connection-settings.png)

Tunatumaini kwamba watumiaji wengi wetu wanaoishi chini ya udhibiti mkali wataweza kuunganisha Tor kwa kubonyeza kitufe, shukrani kwa Connection Assist. Hata hivyo tunajua daima kutakuwa na mizunguko isiyofuata sheria hiyo, na kuna watumiaji wengi ambao wanapendelea kusanidi mawasiliano ya wao wenyewe.

Hivyo ndivyo tulivyowekeza muda katika kubadilisha mipangilio ya Mtandao wa Tor pia - ikionyesha:

  • Jina jipya kabisa: Mipangilio ya Mtandao wa Tor sasa inaitwa Mipangilio ya Uunganisho. Mabadiliko haya yanalenga kufafanua wazi ni vipi mpangilio inavyopatikana katika kurasa hii.
  • Hali ya Uunganisho: Hali yako ya uunganisho wa mwisho inaweza sasa kupatikana juu ya kurasa, pamoja na chaguo la kujaribu uhusiano wako wa mtandao bila kutumia Tor, kwa kutumia Moat, ili kukusaidia kutatua chanzo cha matatizo yako ya uunganisho.
  • -machaguo ya bridge yaliyopo katika sehemu moja:ni orodha ndefu ya vitu na machaguo illiopo kwenye mpangilio wa majibizano ya mtu binafsi, ambayo itasaidia kuboresha.
  • Connection Assist wakati Tor Browser ikiunganishwa na Tor, mtandao haupatikani kutokanana na kudhibitiwa. unaweza tumia njia yingine kuchagua bridge zinazopatikana kiautomatiki.
  • Kadi mpya za bridge: bridges za zamani zilikuwa hazionekani, hata zikiwa zimeundwa. Sasa, bridge zako zilizohifadhiwa zinaonekana kwenye kadi rahisi za bridges -pamoja na chaguzi mpya za kushiriki bridges pia.

Bridge michoro

Hapa ni muundo wa kadi ya bridge inapotanuliwa. pamoja na kuchapisha na kushirikisha mstari wa bridge, kila daraja pia inakuja na nambari ya QR ya pekee ambayo itasomwa na Tor Browser kwenye Android (na programu tumizi zingine zenye nguvu za Tor) katika toleo la baadaye - ikisaidia kuhamisha bridge inayofanya kazi kutoka kwenye kompyuta ya mezani hadi kwenye simu ya mkononi.

Ukiwa na bridges mengi yaliyowekwa, kadi ziitaanguka kuwa rundo - kila moja inaweza kuongezwa tena kwa kubofya. na ikiunganishwa, Tor Browser itakutaarifu ni Bridge gani inafanya kazi kwa sasa ilitumia rangi ya zambarau " ✔ imeunganishwa" pill. Kusaidia kutofautisha kati ya bridges zako bila kuhitaji kulinganisha mistari mirefu, isiyokuwa rafiki ya bridges, tumekuletea bridge-moji: uchoraji wa alama nne fupi unaweza kutumia kutambua bridge sahihi kwa kuangalia kwa haraka.

mwisho, anuani ya msaada ndani ya mipangilio ya uunganisho sasa vinaweza kufanya kazi bila kuwa na muunganisho wa mtandao. Kama ilivyoelezwa hapo awali - kuna aina mbili za viungo vya msaada katika mipangilio ya Tor: zile zinazoelekeza kwenye support.mozilla.org, na zile zinazoelekeza kwenye tb-manual.torproject.org , (yaani, Mwongozo wa Tor Browser). Hata hivyo, tangu web-based sio vya kufaa sana unapokuwa na troublshooting ya mawasiliano na masuala ya Tor Browser, mwongozo sasa umepakuliwa Tor Browser 11.5 na unapatikana bila muunganisho wa mtandao. Zaidi ya viunganishi vya msaada vilivyomo katika mipangilio ya Tor Browser, mwongozo unaweza kupatikana kupitia Menyu ya Programu > Msaada > Mwongozo wa Tor Browser, na kwa kuingiza "about:manual" kwenye mstaruwa anwani ya kivinjari chako pia.

HTTPS-hali pekee, kwa machaguo ya msingi

HTTPS-ony mode]

HTTPS-Everywhere ni moja ya nyongeza mbili ambazo hapo awali zilikuja kwenye Tor Browser, na imeongoza kazi ndefu na yenye mafanikio kulinda watumiaji wetu kwa kuboresha moja kwa moja uhusiano wao kwenye HTTPS popote inapowezekana. Sasa, HTTPS ipo kila mahali, na vivinjari vya wavuti vinavyoongoza vyote vinaunga mkono kiasili cha moja kwa moja hadi HTTPS. kivinjari cha msingi ambacho Tor Browser kinategemea - kinaita kipengele hiki HTTPS-Only Mode.

Kuanzia kwenye Kivinjari cha Tor 11.5, hali ya HTTPS-Only imewezeshwa kwa chaguo-msingi kwenye kompyuta ya mezani, na HTTPS-Everywhere haitakuwa tena ikijumuishwa na Tor Bowser.

Kwa nini sasa? Tafiti ya Mozilla inaonyesha kuwa sehemu ya kurasa zisizo salama iliyotembelewa na watumaji wa wastani ni ndogo – kuzuia usumbufu uliosababishwa na uzoefu wa mtumiaji. zaidi ya hayo, mabadiliko haya yatasaidia kulinda watumiaji wetu kutokana na mashambulizi ya SSL stripping yaliyofanywa na malicious exit relays,na kwa kiasi kikubwa kupunguza msukumo wa kuanzisha exit relays kwa ajili ya mashambulizi ya Man-in-the-Middle.

Unaweza kujua au usijue kuwa HTTPS- Kila sehemu pia hutumika kusudi la pili katika Tor Browser, na ilikuwa ni inawajibika kutengeneza matone salama ya majina ya onion yanayosomeka na binadam. Vizuri, watumiaji wa SecureDrop wanaweza kuwa na uhakika kwamba tumefanya marekebisho kwenye Tor Browser ili kuhakikisha majina ya onion yanayoweza kusomwa na binadamu bado yanafanya kazi hata kama HTTPS-Everywhere haipo.

Kumbuka: Tofauti na kompyuta, Tor Browser kwa Android kitaendelea kutumia HTTPS-Everywhere kwa muda mfupi. Tafadhali angalia sasisho letu tofauti kuhusu Android hapa chini.

msaada wa maandishi yaliyoboreshwa

maandishi yalioboreshwa

Moja ya mikakati mingi ya fingerprinting wa Tor Browser ni kulinda dhidi ya upigaji chapa wa herufi - ambapo mpinzani anaweza kutambua kitambulishi chako kwa kutumia herufi zilizosakinishwa kwenye mfumo wako. kukabiliana na hili, Tor Browser inarahisisha utumiaji wa kawaida wa aina za naneno kutumika badala ya zile zilizosakinishwa kwenye mfumo wako. hata hivyo, baadhi ya maandishi hayakuweza kuonekana vizuri, huku mengine hayakuwa na aina ya maneno yanayopatikana katika Kivinjari cha Tor kabisa.

Kwa kutatua tatizo hili na kupanua idadi ya mifumo ya uandishi inayoungwa mkono na Tor Browser, tumekusanya herufi nyingi zaidi kutoka Noto family katika toleo hili. kiuhalisia , tunapaswa kupata uwiano kati ya idadi ya maandishi ambazo Tor Browser inasaidia bila kuongeza ukubwa wa kisakinishaji sana, jambo ambalo tunalipa kipaumbele sana. Hivyo kama unagundua lugha ambayo herufi zake hazionekani vizuri kwenye Tor Browser tafadhali tujulishe!

tuma mrejesho yako

Ikiwa una mapendekezo juu ya jinsi tunavyoweza kuboresha toleo hili, tafadhali tujulishe. Asante kwa timu zote katika Tor, na kwa wale wengi waliojitolea, ambao wamechangia kwa toleo hili.

Unaitaji msaada?

Angalia FAQ katika jamii yetu

Tembelea Msaada

Wasiliana

wasiliana na sisi moja kwa moja!

Jiunge nasi kwenye IRC